HabariMilele FmSwahili

NCPB yatoa magunia milioni 2 ya mahindi kwa wasaga nafaka nchini

Bei ya unga wa ugali inatarajiwa kushuka, baada ya serikali kuanza kusambaza magunia milioni 2 ya mahindi kwa wasaga nafaka nchini. Muungano wa wasaga nafaka kupitia mwenyekiti wake Peter Kuguru umedhibitisha kupokea taarifa hiyo japo anasema watasubiri hadi jumatatu kuanza kusaga unga.

Anasema kutokana na hili, bei ya unga itashuka kutoka ilivyo kwa sasa shilingi 130.

Kuhusu mpango wa kuagiza mahindi kutoka Tanzania, Kuguru anasema wameusimamisha kwa mudaili  kutumia mahindi waliouziwa na serikali.

 

Show More

Related Articles