HabariMilele FmSwahili

NASA kutangaza mwelekeo wake wa kisiasa leo

Muungano wa NASA unatarajiwa kutangaza mwelekeo wake wa kisiasa hii leo. Kinara wa NASA Raila Odinga aliwahidi wafuase wake kwamba atawaelezea hatua wanazopania kuchukua baada ya kususia uchaguzi wa urais ulioandaliwa wiki jana. Inasubiriwa kuona ni hatua gani Raila atawaelekeza wafuasi wake kuchukua baada ya kuslaia kimya tangu kuandaliwa uchaguzi wa urais alhamisi wiki jana. Akiwatembelea wafuasi wake eneo la Kibra hapa Nairobi siku moja baada ya uchaguzi huo, Raila alisema hatatambua matokeo ya zoezi hilo akidai wakenya wengi hawakushiriki. Tayari Raila ametangaza kubadili muungano wa NASA kuwa vuguvugu linalojulikana kama National Resistance Movement NRM

Show More

Related Articles