HabariMilele FmSwahili

Nairobi yaongoza kwa idadi ya maandamano ambayo yameandaliwa mwaka huu

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa idadi ya maandamano ambayo yameandaliwa mwaka huu.Utafiti wa Article 19 unaonesha maandamano 22 vimenakiliwa Nairobi kati ya Januari hadi Julai. Msimamizi wa Article 19 Kenya,Henry Maina anasema jumla ya visa 80 vya maandamano vimeshuhudiwa kote nchini huku 67 kati yazo yakiwa  maandamano ya amani na 13 yakishuhudiwa ghasia na maafa mawili.Katika utafiti huo ulioshirikisha shirika la IPSOS imebainika pia baadhi ya waandamanaji kushiriki maandamano hayo kwa azimio la kulipwa.Tom Wolf ni mtafiti mkuu wa IPSOS.

Show More

Related Articles