HabariMilele FmSwahili

Naibu Rais Dr Ruto kukutana na makachero wa DCI leo

Kikosi maalum cha makachero kutoka idara ya upelelezi DCI kinatarajiwa kukutana asubuhi hii na naibu rais Dr.William Ruto kufuatia madai ya watu fulani kupanga njama ya kumwangamiza. Mkurugenzi wa DCI George Kinoti anasema alibuni kikosi hicho baada ya Ruto kumpigia simu na kulalamika kwamba watu wasiotaka awanie urais mwaka 2022 wanapanga kumwangamiza. Makachero hao wanalenga kuchukua taarifa kutoka kwa naibu rais ili kuwasaidia kuendesha uchunguzi wao kubaini ukweli wa madai hayo. Tayari mawaziri watatu Peter Munya wa biashara, Joe Mucheru wa mawasiliano na Sicily Kariuki wa afya kutoka Mlima Kenya wameandikisha taarifa baada ya kuhusishwa na njama hiyo ambapo walipuzilia mbali madai hayo.

Show More

Related Articles