HabariMilele FmSwahili

Mwili wa kijana aliyetoweka huko Mwingi, Kitui wapatikana ukioza nyumbani kwake

Mwili wa kijana mmoja aliyeripotiwa kutoweka siku chache zilizopita umepatikana ukiwa umeoza nyumbani kwake  huko Mwingi kaunti ya Kitui.

Mmiliki wa nyumba hizo Mohammed Dondi anasema walilazimika kubomoa mlango baada ya kuanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwenye nyumba yake.

Jirani za marehemu Ali Msenangu wanasema alikuwa katika hali bora ya afya kabla ya kifo chake.

Mwili huo sasa utafanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mwingi level 4 ili kubaini  kilichosababisha kifo chake.

Show More

Related Articles