HabariMilele FmSwahili

Mwanamume azuiliwa kwa kumchinja mwanawe wa mwaka mmoja Bungoma

Mwanaume mmoja anazuiliwa na polisi katika kaunti ya Bungoma kwa madai ya kumuua kwa kumkata kata mwanawe wa mwaka mmoja. Kulingana na naibu chifu wa Tongaren Charles Masika jamaa huyo alimgeukia mtoti wake katika mazingira ya kutatanisa wakati mamake alikuwa shambani.

Masika aidha amearifu kuwa chanzo cha mauaji hayo ya kinyama bado hakijabainika kufikia sasa huku maafisa wa polisi eneo hilo wakianzisha uchunguzi kubaini kilichojiri.

Show More

Related Articles