HabariMilele FmSwahili

Mwanamke anayetuhumiwa kumuiba pacha 1 KNH kusalia rumande kwa siku 5

Mwanamke anayetuhumiwa kumuiba pacha mmoja katika hospitali kuu ya Kenyatta atasalia rumande kwa muda wa siku tano zijazo. Ni baada ya upande wa mashitaka kuiomba mahakama kuwaongezea polisi muda huo ili kukamilisha uchunguzi. Kulingana na upande wa mashitaka uchunguzi umebaini mwanamke huyu ni mwanachama wa kundi linalojihusisha na wizi wa watoto ndani na nje ya jiji la Nairobi. Ednah Kerubo Abuka akijitetea ameiomba mahakama kumwachilia huru akidai alinuia kumrejesha mtoto aliyekuwa amemuiba kwa wazazi wake.

Show More

Related Articles