HabariMilele FmSwahili

Mwanahabari Jackie Maribe aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1

Kesi ya mauaji ya Monica Kimani itaanza Juni 18 hadi 27 mwaka ujao. Jaji wa mahakama ya Milimani James Wakiaga aidha ameridhia ombi la kumuachiliwa kwa dhamana mwanahabari Jackie Maribe.Wakiaga amemtaka Maribe alipe dhamana ya shilingi milioni 1 pesa taslim au bondi ya shilingi milioni 2 na mdhamini wa kiasi sawia. Uhuru wa Maribe Wakiaga anasema umetokana na misingi ni mzazi wa kipekee wa mwanawe wa miaka 4 na kwamba kazi yake kama mtangazaji wa runinga haiwezi kutatiza kesi hiyo kama ulivyodai upande wa mashtaka. Maribe hata hivyo amepigwa marufuku dhidi ya kusoma au kufanya habari yoyote inayohusiana na kesi hii.Mpenzie Joseph Irungu alamarufu Jowie hata hivyo amenyimwa dhamana. Wakiaga akisema anauwezo mkuu kuhitilafiana na uchunguzi

Show More

Related Articles