HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi wa chuo cha JKUAT apigwa risasi na kujeruhiwa baada ya kuingia ikulu ya Nairobi

Mwanafunzi wa mwaka wa 5 katika chuo kikuu cha JKUAT amepigwa risasi na kujeruhiwa baada ya kupanda ua na kuingia katika ikulu ya Nairobi. Kulingana na taarifa kutoka ikulu, mwanafunzi huyo kwa jina Kibet Bera  alitishia maafisa wa polisi kwa kisu alijaribu kuzuiwa hatua iliyosababishwa kupigwa risasi begani. Tukio hilo lilitokea mwendo wa saa kumi jioni jana huku mshukiwa akipelekwa katika kituo cha polisi cha Kileleshwa ambapo baadaye alipelekwa kupokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Uchunguzi unaendelea kubaini kiini cha mshukiwa kuchukua hatua hiyo. Aidha tahadhari imetolewa kwa uumma dhidi ya vitendo kama hivyo.

Show More

Related Articles