HabariMilele FmSwahili

Mwakilishi wa kina mama Zuleikha Hassan afurushwa bungeni baada ya kushiriki vikao na mwanawe mchanga

Mwakilishi wanawake kaunti ya Kwale Zuleikha Hassan amefurushwa bungeni baada ya kushiriki vikao vya asubuhi akiwa na mwanawe mchanga.

Hatua ambayo imesabaratisha vikao  hivyo kwa muda wa dakika 30 kiongozi wa wengi Adan Dualle aliyekuwa na hamaki akishinikiza Zulekha kuadhibiwa. Kulingana na Dualle sheria za bunge ziko wazi na haziruhusi asiyekuwa mbunge kuingia katika majengo hayo.

Uamuzi wa kumfurusha Zuleikha ulizua cheche za maneno miongoni mwa wabunge wa kike walioondoka nje na mtoto wa Zulekha wakidai ni haki ya mama kumlea na kumnyonyesha mwanawe pahala popote pale hata bungeni.

Aidha mbunge mwengine aliyefurushwa na Zulekha kwa utovu wa nidhamu ni Samuel Atandi wa Alego Usonga.

Show More

Related Articles