MichezoMilele FmSwahili

‘Mtundu’ Koscielny abisha hodi Ufaransa na Klabu ya Rennes

Beki mfransa Laurent Koscielny amezidi kuvuruga mipango ya kocha wake Unai Emery hii ni baada ya kubainika kwamba yupo mbioni  kuitaliki klabu hiyo ya London na kuyoyomea Rennes Ufaransa.

Habari kuu Ufaransa ni kuwa,Koscielny mwenye umri wa miaka 33 ameafikia makubaliano na klabu hiyo ya Rennes ikiwa na maana kwamba yupo wima kukamilisha taaluma yake ya miaka 9 akiwa na ‘The Gunners’.

Nahodha huyo alidinda kusafiri na timu kuelekea Marekani kwa mechi za maandalizi ya msimu mpya,Arsenal ikitangaza kumuchukilia hatua za kinidhamu.

Hata hivyo licha ya kuzidisha nia yake ya kughura London,wakuu wa Arsenal wameonekana kumpuuza japo wameeka bei yake kuwa pauni milioni 8.

“Nilijaribu kuzungumza naye mara tatu kabla ya safari ya Marekani ila aliamua kusalia London. Pia nilimwomba azungumze na wakuu wa timu kuhusu uamuzi mwafaka kwake na klabu kwa ujumla na kwa vile amedinda swala, hili lipo mkononi mwake na Klabu kuamua,”amesema kocha Unai Emery

Show More

Related Articles