HabariMilele FmSwahili

Mtihani wa majaribio ya mtaala mpya (CBC) kwa darasa la tatu kuanza leo kote nchini

Mtihani wa kwanza wa majaribio kwa wanafunzi wa darasa la tatu wanaofanya mtaala mpya wa elimu unaanza leo kote nchini.

Waziri wa elimu George Magoha anasema haya ni majaribio ya kubaini iwapo wanafunzi hao wanaelewa mtaala huu wa 2-6-3-3 na yataendelea hadi mwisho wa muhula huu wa tatu.

Waziri Magoha anasema majaribio haya yanayowahusisha wanafunzi milioni 1.3 sio mtihani ila ni mafunzo ya kuisadia serikali kubaini ni wapi kunastahili kufanywa mabadiliko.

Show More

Related Articles