HabariMilele FmSwahili

Mtahiniwa wa darasa la 8 afariki baada ya kuzama katika bwawa la kimao Baringo

Mtahiniwa wa darasa la nane amefariki baada ya kuzama katika bwawa la kimao eneo la Baringo Kusini. inaarifiwa Titus Rono aliyekuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Patkwanin alikuwa akiogelea na wenzake alipozama jana jioni. Babake mtoto huyo Sylvester Kipsoi, anasema alipokea maelezo saa 9 kuhusu kifo chake muda mfupi baada ya mwendazake kusema alinua kwenda kuvua samaki katika bwawa hilo. Akizungumza baada ya kuzuru eneo la mkasa gavana wa Baringo Stanley Kiptis amesema maafisa wa ulinzi watatumwa katika bwawa hilo ili kuwazuia watoto kuogelea bila waelekezaji.

Show More

Related Articles