HabariMilele FmSwahili

Msongamano wa magari washuhudiwa katika barabara ya Naivasha- Mai Mahiu baada ya trela kupata ajali eneo la Lari

Wasafiri katika barabara ya Naivasha Maimahiu wanakabiliwa na wakati mgumu kufuatia msongamano wa magari unaoshuhudiwa katika barabara hiyo kwa sasa. Inadaiwa msongamano huo inasababishwa na trela ambayo imebingiria na kuanguka katika eneo la Kairuri karibu na Lari. Msongamano huo pia umeathiri barabara ya Limuru Mai Mahiu.

Hali sawia ilishuhudiwa mapema leo katika barabara ya Mombasa Nairobi eneo la Tsavo. Msongamano huo unadaiwa kuanza mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia leo pale trela mbili zilipogongana na kuzuia sehemu zote mbili za barabara.

 

Show More

Related Articles