HabariMilele FmSwahili

Jerad Otieno na washukiwa wengine wa biashara ya dhahabu ghushi kuzuiliwa hadi tarehe 27

Mshukiwa mkuu katika sakata ya dhahabu ghushi Jared Otieno na wenzake 16 wataendelea kuzuiliwa hadi tarehe 27 mwezi huu. Hakimu Francis Andayi amekatalia mbali  ombi la kutaka  16 hao kuachiliwa kwa dhamana. Jared na wenzake wameshtakiwa kwa kosa la   kumlaghai raia mmoja wa kigeni kiasi cha shilingi milioni 300. Wanatuhumiwa kutumia vibango bandia  vya biashara ya dhahabu na  wizi.

Show More

Related Articles