HabariMilele FmSwahili

Msaidizi wa Obado,Michael Oyamo kusalia korokoroni kwa siku 14

Msaidizi wa gavana wa Migori Okoth Obado Micheal oyamo atasalia korokoroni kwa siku 14 katika kituo cha polisi cha Muthaiga hapa jijini Nairobi. Hii ni kufuatia agizo la jaji wa mahakama ya Milimani Luka Kimaru kuwa Oyamo azuiliwe ili kuruhusu upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi dhidi yake kuhusiana na mauaji ya Sharon Otieno aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo. Jaji Kimaru ameagiza Oyamo kurejeshwa mahakamani tarehe 26 mwezi huu ambapo huenda akafunguliwa mashtaka ya mauaji. Agizo la jaji Kimaru limefuatia ombi la upande wa mashtaka kwa polisi kuruhhusiwa kukamilisha uchunguzi wa mawasiliano ya simu pamoja na chembe chembe za dna za mshukiwa.Ni ombi lililoridhiwa na familia ya Sharon kupitia wakili Peter Kaluma .Hata hivyo mawakili wa Oyamo June Ashioya na Rodgers Abisai walipinga ombi hilo wakisema polisi wamekuwa na muda wa kutosha kukusanya ushahidi tangu walipomkamata wiki iliyopita.

Show More

Related Articles