HabariMilele FmSwahili

Moto wasababisha hasara katika soko la Gikomba

Wafanyibiashara kadhaa katika soko la Gikomba wanakadiria hasara baada ya moto mkubwa kuteketeza biashara zao. Moto huo unaarifiwa kuzuka mwendo wa saa 10 alfajiri katika eneo linalofahamika kama line 42. Miongonui mwa vibanda vilivyochomeka ni vya wafanyibiashara wa kuuza viatu.Vikosi vya zima moto vimefanikiwa kuuzima baada ya takriban saa 2.

Show More

Related Articles