HabariMilele FmSwahili

Mmoja wa washukiwa wakuu wa kashfa ya dhahabu bandia Jared Otieno akamatwa

Mshukiwa mkuu katika kashfa ya ulanguzi wa dhahabu ghushi nchini Jared Otieno yuko katika makao makuu ya idara ya DCI hapa Nairobi. Otieno alikamatwa kufuatia msako ulioendeshwa na polisi katika makaazi yake mtaani Karen hapa Nairobi. Polisi wamenasa magari mawili ya kifahari katika makazi hayo. Hayo yjkijiri makachero wa DCI wanajipanga kumhoji seneta wa Bungoma Moses Wetangula kuhusiana na biashara hii. Ni baada yake kutajwa miongoni mwa walioendesha biashara ya kuilaghai familia moja ya Emirati milioni 250 kupitia biashara hii.

Show More

Related Articles