HabariMilele FmSwahili

Mmiliki wa bwawa la Patel, Perry Mansukh aachiliwa kwa bondi ya millioni 5

Mmiliki wa bwawa la mauti la Patel huko Solai Perry Mansukh,meneja wake Vinoj Kumar na watu wengine 6 wameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni 5 au mdhamini wa milioni 2.5. Hakimu wa mahakama ya Naivasha amewaagiza washtakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya usafiri mahakamani kesi yao inapoendelea kusikizwa. Wamekua wakizuiliwa tangu alhamisi wiki jana wakikabiliwa na makosa ya kuhusika kwenye mauaji ya watu 48 kufuatia mkasa wa bwawa la Patel kuvunja kingo zake mwezi mei mwaka huu.

Show More

Related Articles