HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa wahudumu wa magari ya teksi za mitandaoni waingia siku ya pili

Wahudumu wa magari ya teksi Digitali wameendelea kugoma kwa siku ya pili mfulilizo kulalamikia kunyanyaswa na wenye kampuni za mitandao. Kwa mujibu wa mwenyekiti wao, Wycliffe Walutalala, kinachowakera zaidi ni wenye kampuni za mitandao kutozingatia mkataba walioweka unaotoa muelekeo wa nauli ya teksi hizo. Kathalika wanalalamikia hatua ya kampuni hizo za mitandao kuruhusu magari mengi na kuifanya vigumu kupata riski ikizingatiwa idadi ya wanaohitaji huduma hiyo haiongezeki.

Sasa wanashikilia hawako tayari kurejea kazini kwani ina hasara tele endapo mamlaka ya ntsa haitaingilia kati kuhakikisha utekelezaji wa mkataba uliopo.

Hayo yakijiri wahudumu wa teksi hizo wanaokiuka wito wa mgomo wanaandamwa na magari yao kuharibiwa, kisa kikiripotiwa eneo la Dagoreti Corner jijini Nairobi.

Show More

Related Articles