HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa wahudumu wa afya kaunti ya Kisumu waingia siku ya nne

Wenyeji wa kaunti ya Kisumu wanalalamikia mgomo wa wahudumu wa afya katika hospitali za umma unaoingia siku yake ya nne hii leo.

Wanadai inawalazimu kusaka huduma za afya katika hospitali za kibinafsi hali wanayosema ni mzigo kwao kugharamia matibabu.

Wanatoa wito kwa gavana wa kaunti hiyo Anyang Nyongo kulipatia mwafaka wa haraka swala hilo.

Wahudumu hao wanashikilia kamwe hawatorejea kazini hadi walipwe mshahara wao.

Show More

Related Articles