HabariMilele FmSwahili

Mcdonald Mariga kubaini iwapo atawania wadhfa wa ubunge Kibra leo

Mwanasoka Mcdonald Mariga atabaini iwapo atawania wadhfa wa ubunge Kibra hii leo.

Kamati ya kutatua mizozo ya tume ya uchaguzi IEBC ikiongozwa na mwenyekiti Wafula Chebukati itatoa mwelekeo kuhusu hatma ya Mariga katika makao makuu ya IEBC yalio kwenye jengo la Annivesary Towers hapa Nairobi.

Mariga alikua amefungiwa nje ya kinyanganyiro hicho kwa madai ya kutojisajili kama mpiga kura hatua iliomlazimu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Akiwasilisha hoja zake kwa IEBC wiki jana,Mariga alisisitiza yeye ni mpiga kura eneo bunge la Starehe.

Show More

Related Articles