HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Starehe Charles Njagua akamatwa

Mbunge wa Starehe Charles Njagua Kanyi, amekamatwa. Njagua amekamatwa muda mfupi uliopita katika majengo ya bunge. Maafisa wa polisi ambao hawakuwa wamevaa sare rasmi ndio wamemchukua Jaguar na anatarajiwa kuandikisha taarifa katika makao makuu ya idara ya jinai DCI .

Aidha akizungumza na Milele Fm muda mfupi kabla ya kutiwa mbaroni, Jaguar amejitenga na madai ya uchochezi. Anasema yuko tayari kuandikisha taarifa kuelezea matamshi yake kwamba wafanyibiashara wa kigeni wanatatiza biashara za wakenya Gikomba.

Tayari tume ya uwiano na utangamano wa taifa NCIC imeelezea Milele Fm kwamba inashirikiana na DCI kumchunguza Jaguar. Afisa mkuu mtendaji Hassan Mohamed anasema wanatarajiwa kumfungulia Jaguar mashtaka mawili ya uchochezi na ubaguzi

Show More

Related Articles