HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Nyakach Aduma Owuor aachiliwa kwa dhamana

Mbunge wa Nyakach Aduma Owuor ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tatu pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni kumi sawa na mdhamini wa kiasi sawa na hicho katika kesi ya ulaghai inayomkabili. Hakimu mkuu wa mahakama ya ufisadi Lawrence Mugambi amemwachilia aduma kwa dhamana hiyo katika kesi ya njama ya kutaka kuipora serikali ya kaunti ya Nairobi shilingi milioni 68 sawa na matumizi mabaya ya afisi. Anadaiwa kupanga njama hii alipohudumu katika  baraza la kaunti ya Nairobi kama mkurugenzi wa masuala ya kisheria awamu iliyopita ya uongozi wa kaunti ya Nairobi. Wakati huo mahakama imemetoa masharti kadhaa kwa Oduma ikiwemo kusalimisha cheti chake cha usafiri kwa mahakama wakati huu kesi ikiendelea kusikilizwa

Show More

Related Articles