HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala afikishwa katika mahakama ya Busia

Mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala yuko kizimbani katika mahakama ya Busia. Wanjala anayekabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo uharibifu wa mali na kumjeruhi afisa wa polisi anasubiri kusomewa mashtaka. Wanjala alikamatwa siku ya Jumamosi baada ya makabiliano kati ya wafuasi wake na wale wa mpinzani wake Ababu Namwamba. Hata hivyo Ababu ametaka kuachiliwa kwake akisema hana kinyongo naye.

Show More

Related Articles