HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Baringo Kusini Grace Kipchoim aaga dunia

Mbunge wa Baringo Kusini Grace Kipchoim ameaga dunia. Kipchoim amefariki mapema leo alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi. Kipchoim amekuwa akiugua ugonjwa wa saratani ya tumbo kwa miaka kadhaa sasa. Itakumbukwa alichaguliwa tena kuwa mbunge wa Baringo Kusini alipokuwa amelazwa hospitalini katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa wa Agosti 8.

Show More

Related Articles