HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Sirisia John Waluke apatikana na hatia ya kuhusika na kashfa ya mahindi

Mbunge wa Sirisia John Waluke amepatikana na hatia ya kuhusika na kashfa ya mahindi ambapo alipookea zaidi ya shilingi 300 milioni kutoka kwa bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao (NCPB). Ni baada ya upande wa mashtaka kudhibitisha waluke pamoja na washtakiwa wengine Grace Wakhungu na kampuni ya Erad walipokea pesa za umma kwa njia ya undanganyifu. Walukhe, na Wakhungu kupitia kampuni yao ya Erad Supplies wanatuhumiwa kula njama za kuilaghai NCPB pesa hizo kwa kuwasilisha cheti cha kudai malipo ya kugharamia uhifadhi wa tani 40,000 za mahindi meupe yaliyokuwa yameiingizwa nchini na kampuni ya Chelsea.

Show More

Related Articles