HabariMilele FmSwahili

Mbadi amshinikiza rais kutia saini sheria ya kuahirisha ushuru kwa bidhaa za mafuta

Kiongozi wa wachache bungeni John Mbadi sasa anamshinikiza rais Uhuru Kenyatta kutia saini sheria ya kuahirisha kwa muda wa miaka 2 utekelezwaji wa ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta.Katika mahojiano na Milele Fm Mbadi anasema iwapo hilo halitoafikiwa basi watalazimika kuandaa mkao wa wabunge wa upinzani kushinikiza kuandaliwa mkao wa bunge upesi ili kumuokoa mkenya.Katika mahojiano na milele fm mbadi kadhalika anapendekeza kupunguzwa bajeti ya mwaka 2018/2019 badala ya kutekelezwa ushuru huo wa asilimia 16. Mbadi anasema hiyo ndio njia ya kipekee kumwokoa mkenya kutokana na mzigo mkubwa wa kuongezeka gharama ya maisha inavyoshuhudiwa wakati huu.

Show More

Related Articles