HabariMilele FmSwahili

Mawaziri 4 walioagizwa kufika DCI kuandikisha taarifa wakana kumtishia maisha naibu wa rais

Mawaziri Peter Munya wa biashara, Secily Kariuki wa afya, Joe Mucheru wa mawasiliano na James Macharia wa uchukuzi wamekana madai ya kupanga njama ya kumwangamiza naibu rais William Ruto. Badala yake wanasema mkutano walioufanya unaodaiwa walitumia kupanga njama hiyo,ulikua wa kujadili lalama za wabunge wa mlima Kenya kuhusu kutelekezwa na serikali kuu kimaendeleo. Akiongea kwa niaba yao baada ya kuhojiwa na makachero wa idara ya upelelezi DCI,Munya ametaja madai hayo kuwa propaganda yasio na  ukweli wowote.Munya anayedaiwa kuongoza vikao hivyo anasema Ruto hajawahi kuibua madai hayo kwao au mbele ya baraza la mawaziri.

Licha ya hili, wanasema wataendelea kufanya kazi na yeye na kwamba hawatakoma kuendelea kukutana kupanga mikakati ya kuwahudumia wakenya

Show More

Related Articles