HabariMilele FmSwahili

Matiang’i akosa kufika mbele ya kamati ya seneti inayochunguza mkasa wa bwawa la Solai

Waziri wa usalama wa ndani amekosa kufika mbele ya kamati ya bunge ya seneti inayochunguza mkasa wa bwawa la Solai lililopelekea vifo vya zaidi ya watu 40. Mwenyekiti wa kamati hiyo seneta Mutula Kilonzo Jr aidha amekosoa vikubwa hatua ya Mataingi kutofika mbele yao bila kujulisha kamati hiyo mapema. Mutula sasa amemtaka Matiangi kufika binafsi mbele ya kamati hiyo kesho saa 5 kueleza ulipofika uchunguzi wa mkasa huo.

Hata hivyo naibu wake Patrick Ntutu amemtetea mkubwa wake akisema aliandika barua kwa spika wa bunge la taifa kumjulisha kwamba hangefika bungeni leo

Wakati huu waziri wa mazingira Keriako Tobiko anawasilisha taarifa yake mbele ya kamati hiyo ambapo anazungumzia ukosefu wa kufuatwa baadhi ya utaratibu kabla ya kuchimbwa bwawa hilo

Show More

Related Articles