HabariMilele FmSwahili

Masanduku 13 ya pesa yaliyotumika kuiba milioni 72 yapatikana kaunti ya Kiambu

Masanduku kumi na tatu ya pesa zilizotumika kuiba shilingi milioni 72  katika mtambo wa pesa almaarufu ATM ya benki za Standard Chartered, CFC Stanbic ,KCB na Barclays  zimepatikana katika msitu wa Thogoto kaunti ya Kiambu.

Sanduku hizo zimepatikana zikiwa bure huku maafisa wakikosa kufanikiwa kumkamata yeyote.

Wezi waliojidai kuwa polisi waliambatana na maafisa wa G4S kupeleka fedha katika eneo la Nairobi West Alhamis  pale pesa hizo zilipoibiwa

Show More

Related Articles