HabariMilele FmSwahili

Marehemu wakili Karanja Kabage kuzikwa leo eneo la Mang’u kaunti ya Nakuru

Mazishi ya marehemu wakili Karanja Kabage yameratibiwa kuandaliwa nyumbani kwake eneo la Mang’u huko Rongai kaunti ya Nakuru hii leo.Mwanawe marehemu Kabage Karanja anasema mwili wa mwendazake utasafirishwa asubuhi hii kutoka hifadhi ya miili ya Lee hapa jijini Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake dk William Ruto pamoja na viongozi wengine serikali na wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayomarehemu kabage alifariki wiki jana baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani karibu na Boma yake iliyoko katika mtaa wa Karen hapa jijini Nairobi

Show More

Related Articles