MichezoMilele FmSwahili

Man United yawinda nyota wa Juventus

Miamba wa soka nchini England Manchester United wamebisha hodi kwa Old Lady Juventus wakiwa na nia moja ya kumchukuwa mpiga magoli Paulo Dybala.

Kulingana ripoti mjini Turin,tayari wakuu wa Man United wamezinduwa gumzo na Juventus kwa malenga ya kumdundisha mkali huyo wa Argentina ugani Old Trafford kabla ya kazi ya msimu mpya.

Dybala mwenye umri wa miaka 25 alifungia mabingwa hao wa ligi kuu Italia magoli 10 msimu uliopita japo amefeli kupata nafasi nyingi za kucheza hususan baada ya ujio wa Christiano Ronaldo aliyeghura Real Madrid 2018.

Inaaminika kwamba Juventus iko tayari kumwachilia mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Palermo na inanuia kumchukua Romelu Lukaku kutoka United

Show More

Related Articles