HabariMilele FmSwahili

Majaji wanaonui kuteuliwa kuhudumu katika mahakama ya rufaa kuhojiwa hadharani

Shughuli ya kuwahoji majaji wanaonuia kuteuliwa kuhudumu katika mahakama ya rufaa sasa itaendeshwa hadharani. Aidha tume ya huduma za mahakama imedhibitisha kubatilisha uamuzi wake wa jana kuwapiga marufuku wanahabari kuangazia vikao vya mahojiano hayo. Hii ni baada ya umma kulalamikia vikali mahojiano hayo kuandaliwa kwenye faragha. Majaji wanne wameratibiwa kufika mbele ya tume ya JSC kuhojiwa katika zoezi hilo litakaloendelea hadi mwezi Julai.

Show More

Related Articles