HabariMilele FmSwahili

Maiti ya mwanafunzi yapatikana chumbani mwake katika chuo kikuu cha Egerton, Njoro

Mwanafunzi wa mwaka wa tano katika chuo kikuu cha Egerton eneo la Njoro amepatikana ameuawa chumbani mwake asuhubi hii. OCPD wa eneo la Njoro Mohammed huka amedhibitisha kisa hicho akisema mwili wa mwanafunzi huyo umekuwa na majeraha ya panga ambayo pia imepatikana chumbani mwake. Mwili wa marehemu aidha umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya chuo kikuu cha Egerton huku uchunguzi ukianzishwa kubaini kilichojiri. Hata hivyo huka anasema wanasubiri ripoti ya upasuaji ya mwili wa mwendazake ili kusaidia katika uchunguzi kumfahamu aliyemuuwa

Show More

Related Articles