HabariMilele FmSwahili

Mahojiano ya kusaka majaji wapya wa mahakama ya rufaa kuanza rasmi leo

Mahojiano ya kuwasaka majaji wapya wa mahakama ya rufaa yanaanza rasmi leo mawakili tajika wakitarajiwa kufika mbele ya tume ya huduma za mahakama. Nyadhifa hizo ziliachwa wazi baada ya kustaafu majaji John Wycliffe Mwera, GBM Kariuki, Festus Azangalala, Anyara Emukule na  Onyango Otieno huku jaji Erastus Githinji akitarajiwa kustaafu mwaka huu. Miongoni mwa wanaowania wadhifa huo ni jaji Justice Hellen Omondi, Christine Meoli, Mary Kasango na  Justice Boaz Olao. Wengine ni majaji Luka Kimaru, Jessie Lesiit, Hedwig Ong’undi, Stephen Radido, Fredrick Ochieng, Joel Ngugi, Joseph Sergon na  francis tuiyot. Katika zoezi litakalodumu miezi 2 JSC pia imeraratibiwa kuwahoji wanaowania wadhifa wa jaji katika mahakama ya kimazingira na ile ya leba.

Show More

Related Articles