HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaamuru shule ya Olympic kumrejesha shuleni mwanafunzi aliyetimuliwa kwa kufuga rasta

Shule ya upili ya Olympic hapa jijini Nairobi imeagizwa kumrejesha shuleni mwanafunzi wa kike wa kidato cha kwanza aliyetimuliwa kwa kufuga rasta.

Jaji Chacha Mwita ameamua usimamizi wa shule hiyo ulikiuka haki za msichana huyo za kuabudu ilipoakataa kumsajili hadi pale atakaponyoa nywele hizo.

Jaji mwita pia ameamua kuwa dhehebu la rastafari linapaswa kuheshimiwa na kulindwa haki za mwanafunzi huyo pamoja na wanachama wengine.

Uamuzi huu unafuatia kesi iliyowasilishwa na babake msichana huyo akidai kubaguliwa bintiye kwa misingi ya kidini.

Show More

Related Articles