HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaagiza kufungwa kwa akaunti za benki za mfanyabiashara Humprey Kariuki

Mahakama imeagiza kufungwa kwa akaunti za benki za mfanyabiashara  mmliki wa kampuni za vileo za Wow Breverages na ile ya East African Limitted Humphrey Kariuki anayekabiliwa na kesi ya kususia kulipa ushuru wa biashara zake.

Mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji aliwasilisha ombi hilo kwa mahakama kutokana na kariuki kukosa kujiwasilisha kwa polisi kama alivyomuagiza majuma kadhaa yaliyopita.

Hakimu mkuu Caroline Nzibe amemtaka Kariuki kuzuiwa kutoa au kuweka fedha zozote katika kaunti zake na zile za biashara zake kutokana na madai amekwepa kulipia ushuru wa hadi shilingi bilioni 41 tangu mwaka 2014. Hadi sasa Kariuki yuko nchini Cyprus ambako pia ni raia.

Show More

Related Articles