HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Busia yamtoza faini ya Laki nne mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala

Mahakama ya Busia imemtoza faini ya laki nne pesa taslim mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala pamoja na watu wengine 4. Wanjala na wenzake wanatuhumiwa kuchochea umma pamoja na makosa mengine 3 wikendi hii huko budalangi. Hata hivyo wanjala na kundi lake walikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu martha nanzushi.

Wakili wa Wanjala, Herman Omiti amelalamikia kiwango cha juu cha thamana aliyotozwa mteja wake akisema hakiambatani na mashtaka wanayohusishwa nayo.
Wanjala alikamatwa Jumamosi kufuatia makabiliana baina ya wafuasi wake na wale wa mpinzani wake Ababu Namwamba. Hata hivyo Ababu anasema hana kinyongo naye.

Show More

Related Articles