HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuamua iwapo Swazuri na watu 10 walioshtakiwa naye wataachiliwa kwa dhamana au la

Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi prof Mohamed Swazuri na watu 10 alioshtakiwa nao kwa tuhuma za ufisadi watabaini leo iwapo wataachiliwa kwa dhamana. Washukiwa hao wamesalia korokoroni wakati wa sherehe za pasaka baada ya kufikishwa mahakamani alhamisi wiki jana. 11 hao tayari wamekana mashtaka ya ulaghai na utumizi mbaya wa mamlaka kuhusiana na kulipwa fidia ya zaidi ya shilingi milini 109 kwa kampuni ya MS Tornado ambayo ardhi yake ilitumika kwa ujenzi wa baabara ya Mombasa Southern Bypass na ya Kipevu Oktoba mwaka 2013.Hakimu mkuu Lawrence Mugambi atatoa uamuzi kuhusu hatma ya Swazuri.

Watumiwa wengine 13 wakiwemo wafanyibiashara waliagizwa kujisalimisha kwa maafisa wa EACC kufikia saa 2 asubuhi hii la sivyo wakamatwe.

Show More

Related Articles