HabariMilele FmSwahili

Madaktari kaunti ya Kisumu waanza mgomo wao

Madaktari kaunti ya Kisumu wametangaza kuanza rasmi mgomo wao rasmi hii leo kulalamikia kile wanakitaja kuwa hatua ya serikali ya kaunti kukosa kutekeleza mkataba wao wa makubaliano wa 2017. Wakizungumza katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga madaktari hao wametuhumu serikali ya Gavana Anyang Nyong’o kudinda kuwapandisha vyeo madaktari  na kutowapa bima ya NHIF.

Mwenyekiti wa madaktari hao  Osuri Kevi ametaka  idara ya DCI na EACC kuanzisha uchunguzi  wa madai ya ufujaji wa fedha katika kaunti ya Kisumu.

Show More

Related Articles