HabariMilele FmSwahili

Maandalizi ya zoezi la sensa yakamilika

Maandalizi yote tayari kwa zoezi la hesabu ya watu hapo kesho yamekamilika.Mkurugenzi wa shirika la hesabu ya watu Zachary Mwangi anasema  maafisa wanaosimamia zoezi hilo  leo wanazuru maeneo watakayosimamia kubaini sehemu zilizo na watu  akisema  usalama wao pia umeimarishwa.

Ameongeza kuwa wanashirikiana na wizara ya teknolojia kuhakikisha  data zinazokusanywa zinasalia kuwa siri.

Kwa upande wake msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna anasema maafisa wa hesabu wataandamana na machifu na maafisa wa usalama.

Anasema walio safarini watahesabiwa kabla au baada ya kukamilisha safari. Oguna ameweka bayana kuwa machifu na maafisa wengine wa serikali watakaoshiriki zoezi hili hawatapokezwa mshahara bali marupurupu ya mchango wao.

Show More

Related Articles