HabariMilele FmSwahili

KUPPET yapongeza mpango wa TSC kuwaajiri walimu wapatao 8,762

Chama cha walimu wa sekondari na vyuo, KUPPET kimepongeza mpango wa TSC kuwaajiri walimu wapatao 8,762. Katibu wa chama hicho tawi la Narok Charles Ngeno anasema hatua hiyo itapiga jeki mpango wa serikali wa kutoa mafunzo bila malipo. Akiwahutubia wahabari, hata hivyo anadai nafasi zilizotengewa kaunti hiyo ni chache, kwani wanahitaji zaidi ya walimu 200 wa sekondari. Ngeno aidha ameisuta tume ya tsc kwa kupuuza pendekezo la bunge la
kuwaajiri walimu 20,000.

Show More

Related Articles