MichezoMilele FmSwahili

Kocha wa AFC Leopards Nikola Kavazovic ahamia klabu ya Free States stars Afrika Kusini

Kocha wa AFC Leopards Nikola Kavazovic amezinduliwa rasmi kama kocha mpya wa klabu ya Free States Stars ya Afrika kusini. Kavazovic raia wa Serbia amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu kufunza klabu hiyo,akijaza nafasi ya kocha wa zamani wa Ingwe Luc Emael.

Hatua hii ni pigo kwa mabingwa mara 13 wa ligi kuu nchini Afc leopards ambao walikuwa na matumaini kwamba kocha huyo angerejea Kenya baada ya kurudi kwao juma moja kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa KPL ili kushughulikia babake aliyedaiwa kuugua.

Hata hivyo haijabainika endapo Ingwe itatafuta kocha mwingine au itasalia na kocha msaidizi wa sasa Marco Vasiljevic.

Klabu hiyo ya KPL ilimtimua mwaajentina Rodolfo Zapata mwishoni mwa msimu jana na kumsajili Kavazovic mwanzoni mwa msimu.

Show More

Related Articles