HabariMilele FmSwahili

KNUT yapendekeza kuwekwa kwa kamera za CCTV katika shule zote za mabweni nchini

Chama cha walimu nchini KNUT kimependekeza kuwekwa kamera za siri yaani CCTV katika shule zote za mabweni nchini ili kukabili utovu wa usalama shuleni. Katika barua aliyoandika katibu wa KNUT Wilson Sossion kwa waziri wa elimu Amina Mohamed, KNUT pia imetaka shule hizo kulindwa na maafisa wa usalama. Walimu hao pia wametaka kujengwa kwa kuta za juu zilizowekwa nyaya za stima, kuwekwa kwa kengele za dharura miongoni mwa mikakati mingine.

Show More

Related Articles