HabariMilele FmSwahili

KHRC yaelekea mahakamani kuzuia waziri wa fedha kuwasilisha makadirio ya bajeti

Matayarisho ya serikali kuwasilisha bungeni bajeti ya mwaka wa kifedha 2019/2020 kesho yamepata pigo. Ni baada ya tume ya kutetea haki za binadamu nchini KHRC kuelekea mahakamani kumzuia waziri wa fedha Henry Rotich kuwasilisha makadirio ya bajeti hiyo. Kulingana na KHRC bajeti haifai kuwasilishwa kwa kuwa bunge halijaidhinisha mswada kuhusu ugavi wa mapato. Kesi hii inawadia wakati kukiwa na mgogoro baina ya bunge na sanate kuhusu kiwango cha fedha zinazopaswa kutengewa kaunti zote 47.

Show More

Related Articles