HabariMilele FmSwahili

Kesi ya mauaji dhidi ya wakili Assa Nyakundi yaahirishwa tena

Kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili wakali Assa Nyakundi imeahirishwa kwa mara nyingine hadi mwezi ujao. Jaji wa mahakama kuu James Wakiaga ameagiza kesi hiyo kusikilizwa na jaji Jessi Lesit Julai 9. Ni baada ya familia Nyakundi kupitia wa John Khaminwa kuomba kesi hiyo kuahirishwa ili kupata muda zaidi wa kuandaa ushahidi wao. Ombi hilo hata hivyo limekataliwa mbali na upande wa mashtaka ukitaja uzito wa kesi hiyo.

Aidha jaji Wakiaga ameagiza pande zote kuendelea kutumiza masharti ya mahakama ya Kiambu ambayo ilmwachilia kwa dhamana ya shilingi laki 3 wakili Nyakundi anayedaiwa kumuua bila kukusudia kwa kumpiga risasi mwae Joseph Nyakundi. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kufeli katika jaribio la kumfungulia Nyakundi mashtaka mapya ya mauaji kwa kukusudia.

Show More

Related Articles