HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga ushindi wa Gavana Waiguru kuskizwa upya

Ni pigo kwa gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru baada ya mahakama ya rufaa kurejesha kesi ya kupinga ushindi wake hadi mahakama ya Kerugoya kesi. Awali mahakama ya rufaa iliagiza kusikizwa tena kwa kesi hiyo iliowasilishwa na mama Martha Karua na kukosoa uamuzi wa mahakama ya Kerugoya kuitupilia mbali. Majaji wa mahakama ya rufaa Mohammed Warsame Daniel Musinga na William Ouko walimtaka Karua kuwasilisha upya kesi hiyo. Karua anadai Waiguru hakuchaguliwa kwa njia ya halali kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

Show More

Related Articles