HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala yatupiliwa mbali

Mahakama kuu ya Busia imetupilia mbali kesi ya kupinga kuchaguliwa mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala. Mahakama hiyo imeamua kuwa hakuna ushahidi wa kudhibitisha kuwa wanjala hakuchaguliwa kihalali. Kesi hiyo iliwasilishwa na mlalamishi Paul Odima akidai uchaguzi ulikumbwa na hitilafu huku visa vya udanganyifu vikishuhudiwa pia wakati wa kampeni.

Show More

Related Articles