HabariMilele FmSwahili

Kenya hupoteza bilioni 33 kila mwaka kutokana na biashara haramu ya petroli

Kenya hupoteza shillingi bilioni 33 kila mwaka kutokana na biashara haramu ya mafuta na petroli nchini. Kulingana na katibu wa wiraza ya Petroli Andrew Kamau asilimia 80 ya biashara za mafuta na petroli nchini ni haramu hali inayowafanya wakenya kuendelea kutumi mafuta yaliyochanganywa. Kamau anasema kaunti za Nairobi na Eldoret zinaongoza kwa vituo haramu vya mafuta. Amesema misako dhidi ya vituo hivyo inaendelea katika kaunti hizo sawia na Kisumu kuwanasa wahusika.

Show More

Related Articles